Ndoa Ina Furaha, Na Maumivu Pia

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kwa kawaida kila mtu anategemea maisha ya ndoa kuwa ya furaha, lakini wakati mwingine yanaweza kuwa ni kinyume chake. Matatizo yanapoanza, matokeo makubwa ya hisia hasi, mathalani uchungu, hofu, moyo kujeruhika, wasiwasi, na hata msongo wa mawazo hujitokeza. Aidha, hisia hasi huweza kuzalisha chuki zaidi, hasira, ugomvi endelevu, usaliti, kununiana,na mawasiliano mabaya ndani ya nyumba.
Endapo changamoto hizi hazitapata ufumbuzi, migogoro mikubwa huanza. Hali hii inaweza kusababisha wanandoa kutengana. Kutengana huanza kidogo kidogo. Huanza kwa kutengana vyumba vya kulala. Baadaye hufikia hatua ya kuachana. Mwishowe, ikibidi hata kupeana talaka.
Chanzo cha maumivu kinaweza kuwa, wivu, ukatili, kupuuzwa, kudharauliwa au kunyanyaswa. Maumivu katika ndoa huleta athari kubwa kwa ustawi wa afya ya akili, mwili, na hata kiroho. Maumivu hayo yanaweza kuwa ya kudumu na baadhi ya athari ni kukosa usingizi, kukosa raha, maumivu ya kichwa, uchovu au matumizi ya dawa za kulevya, pombe, na hatimaye hata kutaka kujidhuru.
Mwanandoa anayepitia magumu hayo, anashauriwa kumwona mnasihi ambaye atampa tiba ya mazungumzo ya ana kwa ana. Kama amefikia hatua ya juu, mathalani sonona, mnasihi atampatia rufaa ya kwenda kwa mtaalamu wa afya ya akili kwa matibabu zaidi.
Hapa tunajifunza kuwa hatutakiwi kukaa na matatizo yoyote mioyoni mwetu. Endapo utakuwa umekerwa, itakupasa uzungumze na mnasihi ili akusaidie kupunguza uchungu unaotokana na matatizo unayopitia. Kamwe usikubali kukaa na mzigo wa machungu moyoni mwako. Usiumie peke yako, shirikisha watu unaowaamini, hususan wanasihi, watakusaidia na utaweza kurudia hali yako ya utulivu wa moyo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection