Usichekelee Msiba Wa Jirani, Kelele Zitakufikia Tu.

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mara nyingi watu wanapokuwa kwenye nafasi fulani huwa wana ile hali ya kujisikia na kuona kuwa maamuzi yao ni sahihi. Hali kadhalika, huwa wanajiona kuwa wana uwezo na haki ya kunyanyasa wenzao pale wanapokuwa na uhitaji.

Ni rahisi sana kwa binadamu kusahau kuwa hali hiyo ya uhitaji inaweza ikawakuta hata wao, wakati wowote ule. Shida humpata kila mtu, hazimfuati mtu mmoja. Hata misiba nayo humpata kila mtu kwani haichagui wala haibagui.

Ukweli ni kwamba, kila aliye chini ya jua hili hupitia shida na matatizo kibao. Kila mtu hupata matatizo kwa wakati wake uliopangwa na Muumba. Kwa hali hiyo usemi huu unafanana na ule usemao ‘leo kwangu, kesho kwako’. Haya mambo huwa ni zamu zamu.

Yatupasa tuwe na huruma pale wenzetu wanapopatwa na shida au matatizo yoyote. Hii ni kutokana na ukweli kwamba hata sisi iko siku hali hiyo itatufika. Matatizo ama shida hajaumbiwa mtu mmoja ama baadhi ya watu fulani katika jamii. Msiba sio lazima kufiwa tu, hata uhitaji huwa ni tatizo unaloweza kulinganisha na msiba.

Mfano hai ni ule wa wastaafu ambao sasa hivi wanapata shida sana kutokana na mfumo ulipo. Wanaosababisha wastaafu wahangaike na kuteseka ni wale waliopo madarakani ambako ndiko kunakotengenezwa mifumo kandamizaji. Waliopo madarakani

husahau kuwa hata wao watakuja kustaafu tu siku moja. Siku ikifika, hawatakuwa na ujanja wa kukwepa.

Tuna mengi ya kujifunza kutokana na usemi huo hapo juu. Kwa kifupi, tnafundishwa umuhimu wa kuwa makini pale tunapokuwa kwenye nafasi za kutoa maamuzi. Yatupasa tuwatendee watu yaliyo mema. Hali kadhalika tunatakiwa kuwasaidia ili tuweze kujenga mahusiano mazuri. Tujitahidi kukwepa usumbufu kwa wengine. Pale tunapokuwa na nafasi kubwa katika jamii, tuhakikishe nafasi hizo hazitutenganishi na jamii inayotuzunguka. Binadamu siyo kisiwa, anaishi na watu, hivyo lazima kuwa na mahusiano ya karibu na binadamu wenzetu. Hayo ndio maisha na taratibu zinazotakiwa kufuatwa na mwanadamu yeyote.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ndoa Ina Furaha, Na Maumivu Pia

Next
Next

Cha Ndugu Hakiwezi Kua Chako, Kiogope