Cha Ndugu Hakiwezi Kua Chako, Kiogope

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Watu wengi hupenda sana kujisifu kutokana na kile alicho nacho ndugu yake. Ni ukweli usiopingika kuwa mtu yeyote hatakiwi kujisifu kwa ajili ya mali ya ndugu yake. Hii ni kutokana na ukweli kuwa vitu hivyo au mali hizo siyo za kwake. Kila mtu yampasa atafute kilicho chake. Kitu kikiwa cha kwako unakuwa na uhuru nacho na unaweza ukafanya nacho chochote unachotaka.

Ukitaka undugu ufe basi jaribu kuwa karibu na mali za ndugu zako. Ukifanya hivyo, utakuwa unakaribisha ugomvi usiokuwa na mwisho. Itafika muda mtakuwa hamuelewani kabisa.

Huo ndio utakuwa mwanzo wa masimango. Mwishowe utaishia kuwatafuta watu ubaya. Utajikuta unasema yule kanifanyia hivi na vile. Cha Shaun, unashindwa kukumbuka ulikotoka. Unabaki kulaumu tu na kujikosesha amani.

Yatupasa tukumbuke walichosema wahenga, ‘Cha mtu mavi, ukikiona kitemee mate’. Tafuta chako na siyo kuringia vya wenzio.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usichekelee Msiba Wa Jirani, Kelele Zitakufikia Tu.

Next
Next

Usimfundishe Mtu Kula Samaki, Mfundishe Kuvua Samaki