Usimfundishe Mtu Kula Samaki, Mfundishe Kuvua Samaki

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha yana namna nyingi ya kuanza. Wapo ambao wanaanza vizuri, lakini hao ni wachache sana. Walio wengi huanza kwa ugumu, lakini baadae hufanikiwa. Kuna wale wanaoanza huku wakiishi kwa wenzao. Tunaweza tukasema hao ni tegemezi.

Utegemezi huo upo wa aina mbalimbali. Kuna wale ambao wanategemea kwa mambo ya shule, wakiwa wanafunzi. Wengine huwa tegemezi wanapoanza kazi, hao wanakuwa wanajiandaa kwa kuelekea kuwa na kipato cha kuweza kupanga chumba. Hao wenye kazi ndio walengwa haswa wa usemi huu. 

Kati ya hao kuna wale ambao husahau kabisa kuwa wanatakiwa kujitegemea wenyewe baada ya muda. Watu hawa huona kuwa wana haki ya kuishi chini ya utegemezi wa wengine. Watu wa aina hii huwa ni wabinafsi na tunaweza kusema kuwa ni wanyonyaji ambao huona raha kutegemea watu wengine kuishi, hata kama wameanza kujiweza ama kujimudu.

Usemi huu una mafunzo kwa wale wanaotegemewa na pia wale tegemezi. Watu tegemezi wanatakiwa wafundishwe namna ya kujitegemea wenyewe. Mara nyingi watu huwa hawapendi kuambiwa, hivyo wanaweza wakakusema vibaya. Lakini hata kama watakusema vibaya, utakuwa umewasaidia kuona umuhimu wa kuanza kujitegemea. Hali kadhalika, na wewe utakuwa umeondokana na mzigo wa kulea tegemezi. 

Kwa wale wanaopenda kuwa tegemezi, wanaaswa kutopenda tabia hiyo ya utegemezi kwa sababu utegemezi unaleta umaskini. Yatupasa tuwe makini, hata kama ni ndugu yako, ni bora umpe mtaji ili naye aweze kupanga maisha yake. Ukiendelea kumlea, utakuwa unamharibu na siyo kumsaidia. 

Wahenga walinena, ‘ndugu mkaliane mbali mkutane kwenye matukio’. Wahenga walikuwa sahihi kwani bila ya kila mtu kukaa kwake, mtakuwa mnagombana kila mara. Wapenda utegemezi, wanaaswa kuacha uvivu na pia hawatakiwi kuogopa maisha. Wanatakiwa kuwa na bidii ya kazi. Waswahili walisema, ‘Mtumai cha ndugu hufa masikini’.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Cha Ndugu Hakiwezi Kua Chako, Kiogope

Next
Next

Kidole Kimoja Hakivunji Chawa