Kidole Kimoja Hakivunji Chawa

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika maisha ushirikiano ni nguzo kubwa sana kwenye nyanja yeyote. Mahali pa kazi pakikosa ushirikiano kunaweza kutokea vurugu inayoweza kusababisha hasara kubwa. Kitakachoonekana ni mashindano ya mara kwa mara ambayo hayana tija. 

Kama vidole vilivyo mkononi vinavyotegemeana, ndivyo binadamu tunavyotakiwa kuishi. Hali hii ya ushirikiano inatakiwa iwepo katika jamii zetu pia. Hata kama unajiona una uwezo sana itafika siku utamuhitaji binadamu mwenzio. Tena utashangaa kwani anaweza kuwa yule yule uliyemuona na kumdharau kuwa hana chochote, ni hohehahe.

Sambamba na usemi huu ni ule usemao mkono mmoja haulei mwana. Kuwa na elimu kumzidi mwenzio ni mgawanyiko tu kwani wote mna umuhimu sawa, kila mtu kwenye nafasi yake. Kila mtu lazima aheshimu nafasi ya mwenzake. Tambua kuwa, bila yeye kushika nafasi ile patakuwa na pengo ambalo litakuwa dhahiri ambalo linaweza kuathiri maendeleo ya mahali hapo. 

Ushirikiano ni muhimu sana katika kila jambo. Tumeumbwa na uwezo ama vipaji tofauti. Kwenye wengi, huwa kuna huyu anayefahamu hili na mwingine anayefahamu lile. Ushirikiano huleta upendo na amani kwenye jamii na maendeleo huja kwa haraka zaidi. Daima tukumbuke kuwa ‘Kidole kimoja hakivunji chawa’.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Usimfundishe Mtu Kula Samaki, Mfundishe Kuvua Samaki

Next
Next

Umaridadi Huficha Umaskini