Umaridadi Huficha Umaskini

Joyce Msai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Umaridadi utakuwezesha kuwa na muonekano unaotaka. Haijalishi kazi ufanyayo bali cha msingi ni kupenda kile unachofanya. Usiruhusu kazi unayofanya iwe kikwazo katika mwonekano unaotaka uwe.

Sote tunatambua kuwa kazi zile za kuajiriwa ziko chache mno hivyo wanaopata hizo kazi pia ni wachache. Kama hivyo ndivyo basi kimbilio kubwa la vijana iwe ni kujiajiri wenyewe kwa kufanya shughuli mbalimbali. Katika shughuli hizo mnaaswa kuendelea kujipenda kwani muonekano mzuri humfanya mtu ajiamini na kujithini. Yakupasa popote ulipo, usijiachie, jijali na uwe unapendeza kwa muonekano wako.

Ni imani yangu hata shughuli za kujiajiri zinahitaji uwe na muonekano unaoeleweka. Ukiwa na muonekano wa kupendeza, utavutia wateja wengi kufuata huduma uitoayo. Watu watajaa kwako badala ya kwenda sehemu nyingine. Pia cha kuzingatia, ni kauli nzuri kwa watu. Muonekano mzuri peke yake hautoshi. Kauli nzuri huvuta wateja. Kamwe tusisahau hilo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Kidole Kimoja Hakivunji Chawa

Next
Next

Tambua Adui Anayekutafuna