Tambua Adui Anayekutafuna

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mtesi wa maisha yako ni wewe mwenyewe ndiyo maana wanasema angalia habari zako kwanza kabla ya kutafuta mambo ya wenzio. Yakupasa kufahamu kwamba unatakiwa kuyatatua yale yanayo kuhusu wewe mwenyewe kabla hujaanza kutatua ya watu wengine.

Tusiwe watu wa kuangalia mambo ya watu wengine na tukaanza kusema ya watu, eti huyu ana hili au yule ana lile ama ana shida sana. Hebu tuwe watu wa kuangalia yanayotuhusu kwanza. Tukifanya hivyo tutaweza kutoka mahali panapotukandamiza. 

Inatubidi tutafakari kwa bidii ili kuweza kujua mambo au masuala yanayotuumiza kabla ya kushughulikia mambo yanayowaumiza watu wengine. Inawezekana matatizo yako yanasababisha watu wengine kuteseka au kuumia. 

Tunaaswa kwenye maandiko matakatifu umuhimu wa kuondoa kwanza boriti lililopo kwenye jicho lako ndipo uweze kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzio. 

Usemi huu unatufundisha kuangalia yako kwanza na tukumbuke mbiu yoyote ile inatakiwa kuanzia nyumbani.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Umaridadi Huficha Umaskini

Next
Next

Chakula cha Mchana Hakikosi Kuni