Chakula cha Mchana Hakikosi Kuni

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kuni ni nishati itokanayo na miti. Nishati hii hutumika kupikia chakula, kuchomea matofali, au kuota kwenye maeneo ya baridi kali.
Usemi huu una maana kubwa sana. Mchana chakula kinapikwa vizuri kwa sababu kuni zinaweza kuokotwa kwa urahisi kwa sababu ya mwanga uliopo. Hali kadhalika, mtu mwenye afya bora anafananishwa na usemi huu kwa sababu anaweza kufanya kazi vizuri kutokana na afya yake kuwa nzuri. Lakini pia usemi huu unafananishwa na kijana mwenye umri mdogo. Vijana huwa wanajiona kuwa wao ni bora zaidi na hujiona kuwa wanaenda na wakati.
Mara nyingi, vijana huwaona wazee wao kama wamepitwa na wakati. Hali kadhalika huwaona wazee kama watu wasioweza chochote na wakati mwingine huwafananisha na usiku wa giza. Kukiwa na giza mtu hawezi kuokota kuni.
Kiuhalisia lakini, kila mtu, awe kijana ama mzee anatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuwa na maisha bora. Kila mtu kwa ngazi yake anao uwezo wa kutekeleza majukumu yaliyo mbele yake. Ukweli ni kwamba, kuna tofauti kati ya vijana na wazee. Kuna mambo ambayo vijana wanaweza lakini wazee hawawezi. Hali kadhalika, kuna mambo wazee wanayaweza vizuri lakini vijana hawawezi. Hivyo mambo ya kutamba kwamba vijana wanaweza au wanajua zaidi kuliko wazee, hayana msingi wala ukweli.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection