Mkono Ukupigao Ndio Ukufunzao

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuonyana ni sehemu ya maisha. Kila mtu katika maisha yake anaweza akapata onyo, ni kawaida kabisa kwa mwanadamu yeyote. Unapopokea onyo na na kulifanyia kazi, unaweza kusonga mbele katika mambo yako uyafanyayo.

Baadhi ya watu huwa hawapendi kuonywa wala kuelekezwa katika jambo lolote. Lakini tukumbuke kuwa tunaishi kwa kutegemeana kama vile vidole vinavyotegemeana kwenye mkono. Kama kidole kimoja kikiondoka kutakuwa na kasoro, na shida inaweza kutokea. Kazi nyingine zinaweza zikakwama kutokana na kasoro hiyo.

Kutokana na usemi huu, tunajifunza umuhimu wa kupokea onyo ama ushauri tunapoishi hapa duniani. Yatupasa tukubali pale tunapoonywa ama kupewa ushauri lakini yatupasa tuyafanyie kazi yale tunayoaswa. Ni dhahiri kuwa hakuna mtu aliye mkamilifu hapa duniani.

Binadamu tumeumbwa tofauti. Unaweza ukakuta huyu anajua kitu fulani zaidi kuliko mtu mwingine. Ndivyo binadamu tulivyoumbwa. Kila mtu ameumbwa na karama yake ambayo ni ya kipekee na hailingani na ya mtu mwingine. Hapo ndipo umuhimu wa kila mtu kwa mwenzie unapokuja. Watu wenye karama tofauti wakitegemeana, kutakuwa na matunda mazuri kutokana na muungano wao. Mkono ukupigao hapa hufananishwa na maonyo anayopewa mtu. Mafunzo hapa tunayachukulia vile mtu anavyoyapokea yale anayoambiwa au anayoshauriwa. Hakuna binadamu asiyehitaji maonyo ama ushauri. Sote hatujakamilika, tunahitajiana. Hivyo kuonyana na kushauriana ni masuala ya msingi sana katika maisha ya mwanadamu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Hasira Hasara

Next
Next

Kujifunza Ni Kila Siku