Hasira Hasara

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mara nyingi katika maisha yetu, baadhi ya watu huwa sio wavumilivu pindi pale wnapopa taarifa mbaya. Jambo linapowafikia wanashindwa kufanya uchunguzi kwanza ili kupata ukweli. Wengi huwa wana maamuzi ya haraka, hali ambayo inaweza kuwafanya watende mambo yasiyopendeza kwenye jamii. Matokeo yake ni vurugu na magomvi na kuweka vikao vya kusutana. Hali hii huweza kusababisha watu kuwa na mahusiano mabaya na hata kununiana bila uhakika wa jambo lenyewe.
Msemo unatufundisha kuwa na hekima katika kuamua jambo na pale tunaposikia jambo, inabidi tufanye uchunguzi kwanza kabla hatujalivalia njuga. Yatupasa tuache hasira kwa sababu inaweza kutufikisha mahali pabaya. Ni vema kuzipokea taarifa tunazopewa kwa umakini na busara kabla hatujachukua maamuzi magumu yanayoweza kuleta mifarakano. Cha msingi, tupokee taarifa zozote vizuri na tuzifanyie kazi kwa kutumia busara
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection