Chanzo Cha Umasikini ni nini?

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ulegevu, uvivu na kutokuwa na bidii katika maisha ni chanzo kikuu cha umaskini. Ili ufanikiwe katika maisha inakubidi ufanye kazi kwa bidii. Usipofanya hivyo maisha yako yatakuwa hayana mwelekeo

Hata Maandiko Matakatifu yanasema ‘asiyefanya kazi na asile’. Yampasa kila mtu ajitume katika kufanya kazi. Endapo tutafanya
kazi kwa ulegevu tutaishia kuwa maskini. Tukitia bidii katika kazi tufanyazo tutafanikiwa na kuwa na kipato cha kuridhisha

Kwa maneno mengine, tunaweza kusema kuwa, bidii katika kazi inalipa. Hivyo tujitahidi ili tuwe mfano wa kuigwa na watu wengine kutokana na kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Wakati mwingine ukizembea kufanya kazi kwa bidii na ukajidanganya kuwa utapata matokeo mazuri katika maisha, utakuwa unajidanganya kwani haitatokea kamwe.

Funzo hapa ni kuwa watu wote, hususan vijana, tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii, na kwa umakini. Inatupasa tujitume, tuache uzembe na tusikate tamaa. Ikibidi, itatupasa tujitoe mhanga ili tuweze kuwa washindi na tupate mahitaji yetu muhimu ya kila siku. Kinyume na hapo, tutajikuta tunaingia kwenye tabia ya kujihusisha na wizi, kubaka au kuwa wadokozi, majambazi au watumiaji wa dawa za kulevya. Aidha, matokeo ya kukosa mahitaji muhimu kunaweza kumfanya mtu akose raha, aishi kwa hofu, wasiwasi, achanganyikiwe na hatimaye kuishia kuwa na msongo wa mawazo na kisha kuwa na sonona. Hivyo, tufanye kazi kwa bidii ili tuweze kuepuka umaskini na athari zake.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mwenda Bure Si Mkaa Bure, Huenda Akaokota

Next
Next

Hasira Hasara