Mwenda Bure Si Mkaa Bure, Huenda Akaokota

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tunaishi katika dunia ya mahangaiko ili kupata riziki ya siku hadi siku. Tunalazimika kujituma kila wakati ili kutimiza malengo yetu. Kwa hali hiyo inabidi kuzunguka zunguka hapa na pale ili kujitafutia chochote kile. Hayo ndio maisha ya mwanadamu yeyote hapa duniani.
Kuna usemi usemao mtembezi hula miguu yake ikiwa na maana unapokuwa unatembea lazima utaokota kitu au utakuta na na watu ambao wanaweza wakawa wa msaada kwako.
Mtu ambaye anajishughulisha kwa kutembea hapa na pale sio sawa na yule anayekaa bure akisubiri riziki imfuate pale alipo.
Usemi huu unatufundisha kujihangaisha na kujishugulisha kwani hiyo ndio ngao ya maisha. Ili maisha yaweze kwenda vizuri lazima tufanye kazi kwa bidii. Juhudi na maarifa ndizo zitakufanya uwe na maendeleo na mambo yako yatakuendea vizuri zaidi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection