Penye Mafundi Hawakosi Wanafunzi

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mahali popote penye neema hapakosi watu. Hilo ni jambo la kawaida katika familia za kiafrika. Penye mafundi ambao wana ujuzi fulani lazima pawepo na wanafunzi au watu wa kujifunza kutoka kwao. Watu husema mkulima mmoja lakini walaji ni wengi. Hayo ndiyo maisha.

Kwenye usemi huu tunajifunza kutokuwa wachoyo kwa wenzetu kwa kile tunachokijua. Kama binadamu, yatupasa tusaidiane pale inapobidi. Kama vile vidole vinavyotegemeana, ndivyo nasi itupasavyo kutegemeana.

Hakuna mtu ambaye anafahamu kila kitu, mambo mengine utayapata kwa wenzio. Hivyo ndivyo maisha yanavyotakiwa kwenda. Cha msingi, ni lazima sote tujue kuwa tunategemeana.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mazoea Kutwaa, Kutoa Ni Vita

Next
Next

Mwenda Bure Si Mkaa Bure, Huenda Akaokota