Tulia na Sikiliza Upate Kuwakuta Waliokutangulia

Simulizi ...
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Katika maisha hatupaswi kuwa na pupa au haraka ya maisha. Watu wengi na hasa vijana wetu huwa wana haraka ya kufanikiwa katika maisha, wengi hukosa subira. Mara nyingi hupenda kutamani maisha ya mafanikio ya wenzao na jinsi walivyo na kutamani kama na wao wangelikuwa na hali kama hizo. Tamaa zao za kutaka kuwa kama ‘yule’ zinawaziba kutambua / kuona ukweli wa jinsi huyo wanayemwona kafanikiwa alivyoanza maisha yake. Pengine alipitia mapito makubwa na mazito sana ambayo yalimfundisha kupambana na kumfikisha hapo alipo. Pengine alipambana hadi akakata tamaa lakini akaendelea kusimama na kuwa imara.
Hakuna mafanikio yanayoanzia juu. Kila jambo lina mwanzo wake na mara nyingi mwanzo huwa ni mgumu. Maisha ndivyo yalivyo. Badala ya kutamani maisha mazuri ya wenzetu yatupasa kuwa karibu na wale ambao wamefanikiwa ili kuweza kujua jinsi walivyoanza na hatimaye kufikia mafanikio waliyoyapata. Ikumbukwe kuwa kila safari ina pa kuanzia. Hakuna fanikio linaloanzia juu. Mapambano ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Maisha si lelemama.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania