Kidogo Huzaa Kikubwa

Simulizi ...
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Msemo huu unaingia kwenye uzuri na ubaya au kwenye faida na hasara. Kwenye uzuri, kwa mfano, bunapojifunza jambo lolote lile la manufaa kwa maisha yako ni lazima uwe hodari na mwenye bidii na uvumilivu pia ili upate matunda mazuri. Lakini hii haina maana kuwa ukianza leo safari utafika leo leo. Mafanikio yanakuja kidogo kidogo, pole pole, ni hatua mwishoni unafikia lengo ulilokusudia.
Kwa upande wa ubaya ni pale unapoingia katika jambo la uharibifu lisilo na manufaa lakini wewe mwenyewe si rahisi kugundua kwa vile unagubikwa na furaha, mfano kunywa pombe, kuvuta sigara, kukopa bila kulipa nk. Unaweza kujikuta ukiendelea na hiyo tabia kidogo kidogo, mwisho wa siku tabia ya kunywa pombe, mfano bia 2 imefikia sanduku zima la bia na hatimaye unaharibikiwa kabisa.
Kwa upande wa faida mtu anaweza akafundishwa kitu na mwalimu na baada ya mafunzo akaendelea yeye mwenyewe kufanya mazoezi. Kwa mfano, wanasihi wote tulifundishwa kutengeneza cheni na hereni za shanga. Mwenzetu mmoja hakuishia pale darasani. Baada ya mafunzo aliendelea kufanya mazoezi kidogo kidogo nyumbani. Leo hii ana uwezo wa kutengeneza na hata kuuza kwa wateja. Tayari ameshajitangaza na hivyo anaendelea kuongeza ujuzi lakini pia kipato kwa ajili ya kuboresha maisha yake.
Upande wa hasara ni pale mtu unapodharau kuanzisha kitu au biashara kwa kuona una mtaji mdogo. Ikumbukwe kuwa wote waliofanikiwa walianza kidogo kidogo mpaka leo wamekuwa wafanya biashara wakubwa. Watu wengi tunakwama hapa, tunatamani kuanza na vikubwa lakini kumbe kila kitu ni hatua ili mradi uwe na lengo na nia thabiti.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania