Dalili Ya Mvua Ni Mawingu

Simulizi ...
by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).
Dalili ni alama zinazotambulisha kitu fulani kwamba kimekuja, kinakuja au kitakuja. Dalili zipo za aina mbalimbali, kama vile dalili za magonjwa, mvua, ukame, ugomvi nk. Msemo huu unatukumbusha umuhimu wa kusoma alama za nyakati. Kusoma alama za nyakati haina maana ya kuziangalia saa zetu za mikononi au za kwenye simu zetu. Ni kuangalia matendo yetu ya sasa na hivyo basi umuhimu wa kuzisoma dalili za mambo yatakayotokea.
Mathalani, tuangalie hali ya mahusiano yaliyopo baina ya watu hapa nchini siku hizi. Upendo baina ya watu na watu umetoweka. Wahenga wanasema zamani mtoto alikuwa ni mtoto wa kila mtu, lilikuwa ni jukumu la jamii kumfundisha na kumkanya wakati wowote ilipobidi. Endapo mtoto ama kijana au mtu yeyote ndani ya jamii alipata shida ama tatizo aliweza kukimbilia kwa mwana jamii na kumweleza yaliyokuwa yanamsibu. Ile kupata fursa kuongea ya moyoni kulisaidia sana kupunguza msongo wa mawazo ambao ungeweza kuwa ni changamoto kubwa hapo mbeleni.
Lakini kadiri miaka ilivyokuwa inaenda hali hii ya umoja ilianza kupungua. Hali hii ilipoanza kujitokeza jamii ilikaa kimya tu na kuanza kuizoea hali hiyo. Mtoto alianza kuwa ni wa familia tu na siyo wa jamii tena. Kila mtu alianza kuangalia ustaarabu wake. Hata mtu akipata tatizo inambidi afe nalo, anakuwa hana mahali pa kukimbilia.
Upendo kuanza kutoweka katika jamii ilikuwa inaashiria kitu fulani. Pamoja na kwamba hali hiyo tuliiona, hatukuchukua tahadhari, hatukulishughulikia tatizo hilo, tulikaa kimya.
Dalili mbaya zilianza kuonekana, waliozidiwa na msongo wa mawazo wakaanza kukata tamaa na maisha. Wakaona hakuna sababu ya kuendelea kuishi, uamuzi ukawa ni kuondoa uhai wao. Vito vitokanavyo na watu kujiua vikaanza kujitokeza, mwezi baada ya mwezi, wiki baada ya wiki na leo hii imekuwa siku baada ya siku.
Nini tunajifunza kutokana na maelezo haya?
- Dalili za jamii kuanza kumeguka zilianza kuonekana muda mrefu tu, hatukufanya chochote. Sasa tunajikuta pabaya.
- Thamani ya wahenga kwenye jamii itambuliwe ili kupunguza Vito vitokanavyo na watu kujiua ama kuua
- Jamii iwe na utayari wa kushughulikia dalili ambazo endapo zitaachwa bila kudhibitiwa zinaweza kuleta madhara makubwa.
Ikumbukwe kuwa dalili ya mvua ni mawingu. Yatupasa kujitahidi kuzidhibiti dalili mbaya pale zinapoanza kujitokeza ili kukwepa maafa huko mbele.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania