Mtoto Umleavyo Ndivyo Akuavyo

Simulizi
by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).
Mtoto yeyote yule huwa vile na kukua vile kutokana na jinsi alivyolelewa na wazazi wake. Endapo atalelewa vizuri ndivyo atakavyokuwa, ndivyo atakavyoonekana mbele za watu. Mtoto akilelewa vibaya, matendo yake mbele za watu hayatakuwa mazuri. Atakuwa ni mtoto asiye na adabu, asiye na heshima kwa mtu yeyote.
Mara nyingi msemo huu hutumiwa kuwahimiza wazazi wawape malezi mema watoto wao, malezi ambayo yatawawezesha watoto wao wawe na adabu njema kwa kila mtu.
Hali kadhalika, msemo huu hutumika pia kumuasa mtoto ambaye anaonakana kuwa hana adabu ama hana tabia njema. Ukweli ni kwamba pamoja na kuwa lawama za utovu wa nidhamu zitaelekezwa kwa mtoto, ni dhahiri kuwa wazazi watabeba mzigo mkubwa zaidi wa lawama. Wataambiwa dhahiri kuwa malezi waliyowapa watoto wao ni mabaya na ndio maana watoto wao wako hivyo walivyo, watoto ambao hawakubaliki katika jamii.
Fundisho kwa wazazi wote ni kuwalea watoto wao vile ipasavyo ili wawe na adabu na wasiwe kero kwenye jamii zao.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania