Ya Kale Ni Dhababu

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Mara nyingi binadamu huwa na tabia ya kudharau wazee, hii ni pamoja na watoto kudharau wazazi wao. Husikitisha sana pale unapoona mtoto anawadharau wazazi wake, eti kwa sababu wamekuwa wazee. Ni vema tukajua kuwa kuzeeka ni moja ya mapito ya binadamu wote, na hata wao siku moja watazeeka.

Kwa kawaida, mtu akizeeka haina maana utu/ubora wake unaisha ama unapungua, labda awe amepitiwa na magonjwa ambayo yamemfanya akili zake ziathirike. Hivyo endapo mtu au mzazi amezeeka, anakuwa amezeeka mwili tu lakini siyo akili yake, hekima na busara zake zinabaki pale pale, na pengine kutokana na kuona mengi katika maisha yake anakuwa na hekima nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Hivyo kama mtoto, yakupasa usikilize, uzijali na uzizingatie kwa makini, busara zitakazotoka kwenye kinywa cha mzazi wako ama sivyo utakuwa unajichimbia kaburi lako.

Kizazi cha leo kimekosa maadili kwa sababu ya kudharau ya wazazi au mambo ambayo wazee wao wanawaasa nayo. Mara nyingi huwaona wazee wao na hata kuwasema kuwa wamepitwa na wakati, na wao kujiona kuwa wako juu na wanajua zaidi ya wazee wao. Hiyo siyo kweli hata kidogo, kama msemo huu usemavyo: “Hata siku moja, sikio la binadamu haliwezi likakua kuzidi kichwa chake.”

Vijana wanaaswa kuwasikiliza wazee wao ili wapunguze misongo ya mawazo pamoja na matatizo mengine ya maisha. Wasipozingatia haya wanaweza wakakosa baraka katika maisha yao ya hapa duniani na hata ya Mbinguni. Mzazi ni mzazi, hafananishwi na mtu yeyote. Tuzingatie msemo usemao: “Old is Gold”.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO’s mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy

Previous
Previous

Kuomba Msaada, Kukopa Na Kurudia Makosa Sio Vibaya

Next
Next

Samaki Mmoja Akioza, Wote Wameoza?