Heri Kufa Macho Kuliko Kufa Moyo

Masimulizi
by Susan Njana (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa na kipato duni. Alikuwa anapenda maisha ya anasa sana. Kutokana na kupenda starehe, hali ambayo haikuwa ndani ya uwezo wake, alijibadilisha na kujifanya aonekane ni wa matawi ya juu na hivyo kupapatikia raha ambazo ni za msimu.
Alijitahidi sana kutafuta kila njia ili apate atakacho. Hatimaye alianza mahusiano na mama mmoja ambaye alikuwa tajiri, akawa anamsaidia. Misaada ya huyu mama ilimfanya kijana ajione
kuwa ‘ameukata’, akamshukuru Mungu kwa ngekewa aliyopata.
Ilitokea kwamba mama huyu tajiri alikuwa ameachana na mume wake. Alikuwa na shauku ya kumpata kijana ‘mbichi' ili aweze kukidhi kiu yake ya mapenzi. Hivyo wote wawili (mama na kijana), kwa malengo tofauti walitimiza azma zao, kijana akitak utajiri naye mama akitaka kujifurahisha kimapenzi. Kwa mwendo huu, wawili hawa walikubaliana na hivyo ngoma ikawa ‘draw’.
Baada ya muda mrefu kupita, yapata mwaka moja na nusu hivi, mume wa yule mama aliaamua kumrudia mkewe, alimuomba mke wake wasameheane ili warudiane waweze kuishi kama zamani. Walitambua kuwa hakuna mwanadamu aliyekamilika. Wawili hao wakarudiana na kuanza kuishi pamoja tena kama zamani.
Kijana aliachwa solemba akiwa amekufa moyo kwa pigo hilo zito. Ghafla, maisha ya ‘dezo’ kwa kijana huyu kutoka kwa mama tajiri yalikatika. Alianza kuishi maisha ya taabu, starehe zikaisha. Kwa hakika, alijuta kuzaliwa alipoona anarudia hali yake ya zamani iliyojaa ufukara na mateso ya kukosa kile atakacho kiurahisi.
Tunajifunza nini kutoka kisa hiki?
- Tusitamani vitu ambavyo hatuna uwezo navyo. Waswahili husema, ‘Tamaa Mbele, Mauti Nyuma.’ Kijana aliishia kujuta, kujuta kweli kweli.
- Hakuna njia ya mkato kwenye maisha. Yatupasa kufanya kazi kwa bidii ili tuweze kupata kile tunachostahili.
- Vijana wanaaswa waepukane na vishawishi vya maisha. Isiwe kila kinachoonwa na macho basi moyo unatamani. Ni hatari! Utatamani vingapi? Macho yanaweza kuuponza moyo na hatimaye ukaishia pabaya.
- Pia vijana wanaswa kuwa wavumilivu kwenye maisha. Wahenga walisema, ‘Mvumilivu Hula Mbivu’. Acheni kupapatikia ama kutamani anasa msisoziweza. Kwenye simulizi hii, kijana aliishia kwa kufa moyo.
Usemi wa ‘Heri Kufa Macho Kuliko Kufa Moyo’ una maana kubwa sana katika maisha yetu. Ukitamani kila unachoona, utaishia kufa moyo pale itakaposhindikana kuendelea kuwa nacho kile ulichotamani.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania