Kunyamaza Ni Dawa

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Binadamu tumeumbwa tofauti. Siyo lazima matendo yetu, tabia zetu, utu wetu na mengine mengi yashabihiane na watu wengine. Kukubaliana ama kutokubaliana ni jambo la kawaida kabisa. Mara nyingi panapotokea kutoelewana kati ya pande mbili, mathalani, kati ya mume na mke, kila mmoja anakuwa na jaziba, kuongea au kujibu anavyojisikia ili mradi kila mtu atetee upande wake na aonekane kuwa ni mshindi.

Ni ubinadamu usiopingika kuwa hakuna anayekubali mwenzake aonekane yuko sahihi, yaani hana makosa. Mfano mzuri ni kwa wanandoa. Endapo kunatokea jambo, mke ataongea kivyake, na mume naye ataongea kivyake. Ni kawaida kwa kila mtu kujitetea, hata kama mwenye kosa anajijua vizuri kuwa ni mkosaji. Pamoja na kujijua huko, bado huwa ni vigumu kukiri, kwa sababu tabia ya kubishana imekuwa ni mazoea.

Wenye busara, mara nyingine, huona ni bora kunyamaza tu, kwani kuendelea kuongea au kujibu hakutaweza kumaliza mabishano yaliyopo kati yao. Kuna wakati mwingine unapobishana na mwenzako, yakupasa uangalie sana maongezi yenu yanaelekea wapi. Pengine njia mojawapo inaweza kuwa ni kunyamaza, hiyo inaweza kuwa dawa tosha. Siyo lazima kila anachosema mwenzio ukitafutie majibu, ukifanya hivyo unaweza kujikuta unajibu kitu ambacho kitalifanya jambo lionekane kuwa ni kubwa kuliko lilivyo.

Angalizo kwa akina mama. Wanawake wengi tunapenda sana kubishana na kujibu jibu, mara nyingine bila mpangilio kwa kudhani kwamba utayamaliza salama masuala yanayowakabili. Lakini hii haina maana kuwa tukiulizwa tusijibu. Siyo kila wakati panapotokea hali ya kutoelewana tuongee, tujaribu/tujitahidi kukaa kimya ili kuepusha shari. Mara nyingi, kimya huwa inasaidia sana. Endapo itatokea siku ambayo utaiona kuwa haitakuwa na athari wala tafrani ya aina yoyote kama ukizungumza, fanya hivyo ili uweze kuyatoa yale yakuumizayo. Tukumbuke kuwa kuna athari ya kurundika vitu moyoni bila ya kuvitoa. Msongo wa mawazo ni adui mkubwa sana wa afya yako ya akili. Tuzungumze, lakini kwa mpangilio ili kukwepa mabishano yasiyokuwa na tija, mabishano yasiyojenga, zaidi ya kubomoa.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Adui Yako Ni Yule Uliyemsaidia

Next
Next

Heri Kufa Macho Kuliko Kufa Moyo