Adui Yako Ni Yule Uliyemsaidia

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Katika maisha ya siku hadi siku, mara nyingi tunapenda sana kusaidiana, awe ni ndugu au rafiki. Lakini kubali usikubali ni wachache sana ambao huwa wanakuja kurudisha fadhila au kukumbuka yale waliyotendewa.
Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa ameolewa na baba mmoja ambaye alikuwa ameondokewa na mke wake. Alikuwa mgani. Alikuwa ameachiwa watoto wadogo sana ambao walikuwa bado wanahitaji malezi ya mama. Hivyo mama huyu alikuwa anakuja kuziba pengo lililoachwa na marehemu. Kwa bahati nzuri mama huyu aliwalea wale watoto kama vile wa kwake. Alijitahidi kufanya kila aina ya biashara ili watoto wale waweze kusoma. Kwa kweli watoto hao walisoma vizuri na mwingine hadi kufikia ngazi ya udaktari.
Mwanzoni, watoto hawa walikuwa wanampenda yule mama. Ujio wa mama huyu kwenye nyumba ile ulileta baraka kubwa sana. Wakati anaolewa, mume wake na watoto wake walikuwa wakiishi kwenye nyumba ya kupanga. Wana ndoa hawa, kwa pamoja walipambana mpaka wakawa na uwezo wa kujenga nyumba ya kwao wenyewe Kijichi. Kusema kweli, mafanikio hayo yaliletwa na huyu mama ambaye alikuwa ni mchakarikaji na mtafutaji mkubwa. Kwa kweli maisha yao yalibadilika na kuwa mazuri kuliko hapo awali, kuliko walivyotegemea.
Cha kushangaza lakini, wale watoto ambao huyu mama wa kambo alikazana kuwasomesha kwa hali na mali hata kuwafikisha hapo walipo, waligeuka na kuwa mwiba kwake. Walithubutu hata kumwambia kuwa hana chake pale Kijichi, na kwamba afunge virago vyake, aondoke.
Bahati nzuri huyu mama naye alijaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume ambaye alimsomesha hadi kufikia ngazi ya elimu ya chuo. Bahati yake alikuwa amewekeza kwa kumpatia elimu mtoto wake. Kwa maana hiyo, masimango ya wale watoto wa kambo hayakumtisha sana. Aliendelea na jitihada zake za kupambana ili kutengeneza maisha yake na ya mtoto wake. Mambo yalianza kumuendea vizuri kiasi kwamba aliweza kuondoka hapo nyumbani kama alivyoamriwa na wale watoto wa kambo. Alitaka kukwepa manyanyaso ambayo yalikuwa yamemchosha. Alikuwa amejiandaa kisawasawa kwenda kuishi maisha yake na mtoto wake mahali pengine kabisa. Alifanikiwa.
Kisa hiki ni fundisho kwa wanawake. Tunashauriwa kuwa tunapoingia kwenye nyumba ambayo tayari ina familia, yatupasa kuwa makini na kujitahidi kutafuta kilicho chako. Usidanganyike na mapenzi ya awali kati ya mume na mke. Mapenzi hayo yanaweza kutoweka mara watoto uliowakuta hapo nyumbani wakianza kukubadilikia. Waswahili husema, mtoto wa mwenzio ni wa mwenzio, hata ufanyeje hataweza kuwa kama mwanao wa kumzaa. Usemi wa ‘Kikulacho ki nguoni mwako’ pia ni sahihi kabisa. Hata siku moja mama huyu hakutegemea kuwa itakuwepo siku ambayo watoto wa mume wake wangemgeuka na kuwa kama wanyama kwake. Alikuwa amewahangaikua mno. Mara nyingi, yule unayemsaidia ndio huyo huyo.atakuja kuwa adui yako na kuweza kukumaliza kabisa. Kwenye maisha, yatupasa tuwe waangalifu sana, tusijisahau.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania