Mwenye Kisu Kikali Ndiye Atakayekula Nyama

Joyce Msai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Joyce Msai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kisu ni kitendea kazi ambacho kinapatikana kwenye kila nyumba. Kisu kinatumika kwa matumizi ya nyumbani, shambani na hata katika uwindaji. Hali kadhalika, kisu kinatumika kama silaha ya kujilinda na hata kinyume chake. Wengine hutumia kisu kwa kuondoa uhai wa watu, kitu ambacho si kizuri. Kwa kifupi, kisu ni muhimu kuwepo kila nyumba, ni silaha na ina matumizi mbalimbali.

Ili kiweze kufanya kazi kusudiwa, ni lazima kisu kinolewa kwa ajili ya kufanya kazi tofauti tofauti. Mathalani, katika maisha yetu kuna fursa nyingi sana zinazoweza kutuinua kimaisha na kutupa mafanikio. Kwa vijana, fursa nyingi ziko wazi, kinachotakiwa, ni UBUNIFU.

Hivyo basi maaarifa, bidii na juhudi ndiyo kisu cha mafanikio. Tuvinoe visu vyetu kwa ajili ya fursa mbalimbali ili tuweze kufanikiwa na kutimiza malengo yetu. Maisha yetu hayana fomula, cha msingi ni kuwa wabunifu ili kuweza kupambana na changamoto nyingi zilizopo mbele yetu. Kama wahenga wanavyonena, ‘Mwenye Kisu Kikali Ndiye Atakayekula Nyama,’ ina maana, mwenye kunoa kisu chake ndiye atakayefanikiwa. Hivyo hima kwa kila mtu, hususan vijana kunoa visu vyenu kwa mafanikio yenu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Ukibebwa, Bebeka

Next
Next

Cheka Nao Uwajue Hila Zao