Mafanikio Yanahitaji Uwajibikaji

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Katika maisha ukiona mtu amefanikiwa ujue anawajibika vilivyo. Anakuwa amepitia changamoto nyingi pia, kwa watu wasiojua alikotoka, wanaweza wakasema mengi juu yake, mara hili, mara lile, ili mradi waweze kusema lolote pasi kuwa na taarifa za kutosha kuhusu huyo wamsemaye.
Mfano mzuri, sisi wana tewwy tumefundishwa ujasiriamali, lakini wengi hatuufanyii kazi. Mathalani, tulifundishwa kutengeneza sabuni za maji na shanga. Hivi karibuni tumeletewa unyunyu (perfume) na watu ambao wanatambua na kuzienzi kazi tunazofanya, kazi za unasihi kwa watu wenye matatizo ya afya ya akili. Kwa hakika tunaweza kusema kuwa hizo zote ni fursa kwetu. Ninaamini kuwa kama mafunzo hayo tungeyafanyia kazi, pengine sasa hivi tungeweza kuwa na vijimiradi vidogo vidogo ambavyo vingetusogeza kidogo kiuchumi.
Kama wakina mama tuliostaafu, tungeweza kutumia fursa tunazozipata, na kufanya yale tunayofundishwa ama kuwezeshwa, kwa hakika tungekuwa mbali. Yatupasa kupambana la sivyo hatuwezi kufika. Tukumbuke kuwa maamuzi ya kufanya jambo lolote linahitaji uthubutu. Kamwe tusikate tamaa, hima tusonge mbele ili kuweza kutekeleza yale tuliyoyapanga kwa faida ya watanzania.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania