Huruma Ni Aghali Ila Mungu Ni Mfariji

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Msemo huu una ukweli na uhalisia ndani yake. Ni kawaida kabisa pale mtu anapomsaidia mtu mwingine, hujitoa kwa moyo bila kujali athari zinazoweza kutokea baadaye. Endapo kunaweza kutokea athari, basi Mungu wake huja kumfariji.

Siku moja baba mmoja alikuwa anaenda kazini akiwa anaendesha pikipiki. Ghafla, alimwona dada mmoja kalala barabarani, akiwa hajiwezi. Kama binadamu yeyote mwenye utu na huruma, alisimama, ikabidi ambebe ili ampeleke hospitali. Aliipotembea hatua chache aliona pikipiki yake inaondoka na mtu mwingine. Alipoona vile, yule baba kwa haraka alimuweke dada yule chini, akamkimbiza mwizi wa pikipiki yake bila mafanikio. 

Cha kushangaza na ajabu kweli kweli, aliporudi pale alipokuwa amemuacha yule dada, hakumkuta. Loh, kumbe ulikuwa umefanyika mchezo mchafu. Alikata tamaa ya kupata tena chombo chake. 

Yule mwizi na dada walikutana mbele kwa mbele. Dada alipanda pikipiki, lakini ilikataa kuwaka. Yule mwizi wa pikipiki alimwambia dada ashuke kwanza ili aangalie nini cha kufanya. Dada alipata wasiwasi, alihisi pengine yule jamaa yake alikuwa anataka kumuacha. Kwa hasira, alichukua gogo akampiga nalo kichwani hadi akazirai. Kisha aliondoka kwa haraka mahali hapo. 

Alipanda pikipiki, akaiwasha na kuanza kuendesha. Kwa bahati mbaya hakuweza, ilishindikana kabisa. Wakati huo mwenye pikipiki alikuwa anatembea barabarani huku akiwa amechanganyikiwa. Ghafla, alimuona yule dada akiwa amepanda pikipiki na mwizi wake akiwa kalala kando kando ya barabara. Yule dada alipomuona mwenye pikipiki, alitaharuki na kuiacha pikipiki ile na kukimbia nduki.

Yule baba alipoipata pikipiki yake, hakuwa na ghadhabu bali alimshukuru Mungu, akaondoka zake. 

Kisa mkasa hiki kinatufundisha kutenda wema na kuwasaidia wenye shida. Mungu wetu ndiye mfariji. Methali nyingine zinazoendana na funzo hili ni, “Tenda wema uende zako, usingoje shukurani,” na nyingine pia ni "Wema hauozi."

Kwa hakika ukimtendea mtu wema, ipo siku utapata malipo yake. Waswahili pia husema “Malipo ni hapa hapa duniani.” Huyu mwenye pikipiki ambaye alikuwa na nia ya dhati kabisa ya kumsaidia yule dada, alipata malipo yake hapa hapa na wale hasidi zake nao walipata haki yao hapa hapa pia. Dunia ni mviringo, inazunguka

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Nidhamu Na Taratibu Katika Maisha

Next
Next

Sio Kila Wakati Mume Ana Makosa