Maandalizi Mazuri Ya Kesho Ni Kufanya Vizuri Leo

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mara nyingi katika maisha yetu, binadamu tunaishi kwa kuangalia au kufanyia kazi mambo ya jana badala ya kuangalia nini kifanyike siku ya leo. Kwa mtizamo huo, tulio wengi tunashindwa kumudu maisha. Kama kuna mtu alikukosea, unalifanya kuwa ni jambo la kuhadithia kwa kila umuonaye. Ni lazima uelewe kuwa, kila mtu atakupa ushauri wake ambao unaweza kuwa hasi au chanya. Kwa kawaida, binadamu wengi huwa hawana ushauri wa kumsaidia mtu zaidi ya kumuangamiza. Yatupasa kuwa makini katika hilo na tusiishi kama jana bali tuishi kama leo kwa sababu siku ya leo ni mpya na mambo yake n mapya. 

Yatupasa kukiri kuwa leo ni siku yangu ya kushinda na ndivyo itakavyokuwa kesho yangu. Maandalizi ya leo ni mafanikio yako kesho. Tujifunze kujinenea mazuri siku zote za maisha yetu. Waswahili husema, ‘Kinywa kinaumba’, ukijinenea mema yatakupata mema na ukijinenea mabaya, vivyo hivyo, mabaya ndiyo yatakayokupata.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Wazazi Tusihalalishe Matendo Maovu Kwa Watoto Wetu

Next
Next

Nidhamu Na Taratibu Katika Maisha