Isiyokuwasha, Hujailamba

Simulizi
by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).
Ikiwa kitu kinajulikana na watu wengi kuwa kinawasha, kwa mfano pilipili au kitu kichungu, kwa mfano, shubili, na wewe ukasema hakiwashi au siyo kichungu, hiyo ni dalili kuwa hujakionja au kukiramba kitu hicho.
Usemi huu hutumiwa kumfahamisha mtu anayepinga linalosemwa na wanaojua. Mtu huyo anatakiwa asipingepinge bure. Ni bora achunguze hilo analoambiwa kwanza kabla ya kupinga. Ikiwa ataendelea kupinga, basi itaonyesha kuwa hilo jambo halijui vilivyo au halijampata (hajaliramba). Hao wanaolisema, wao wanalijua maana wameshaliona au pengine, limeshawapata.
Usemi huu unaweza linganishwa na ule usemao, “pilipili usiyoila yakuwashia nini? Semi zote mbili hutumiwa kutufundisha tusiingilie au tusikasirishwe na jambo lisilotuhusu. Maana jambo lisilokuhusu ni kama pilipili usiyoila, vipi itakuwasha?
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania