Nyumba Nzuri Si Mlango

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).

Nyumba yaweza kuwa mbaya, ikawa na mlango mzuri. Hali kadhalika, nyumba yaweza kuwa nzuri lakini ikawa na mlango mbaya. Kwa hiyo huwezi kuijua nyumba kama ni mbaya au ni nzuri, mpaka uingie ndani. Kuangalia mlango wa nyumba peke yake hakutoshi kutoa maamuzi ya uzuri ama ubaya wa nyumba hiyo. 

Usemi huu hutumiwa kuonyesha kwamba huwezi kujua kama kitu fulani au mtu fulani ni mzuri ama ni mbaya kwa kumtazama kwa nje tu, yaani sura yake, mavazi yake, umbile lake na kadhalika. Ni lazima uangalie na vigezo vingine kwa undani zaidi, kama vile tabia yake, utu wake, haiba yake na heshima yake na kadhalika, hapo ndipo utakapomjua kama kweli ni mzuri na anastahili kuitwa hivyo ama la.

Binadamu tulio wengi, tumezoea kuangalia mambo ama watu kijuu juu tu, hiyo si sahihi hata kidogo. Yatupasa tuingie kwa undani zaidi kabla hatujasema mtu huyu ni mbaya ama ni mzuri, hali kadhalika kama kitu hiki ni kibaya ama ni kizuri. Tujifunze kufanya maamuzi ya kina.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Chawa Si Mzito Lakini Husumbua

Next
Next

Radhi Ni Bora Kuliko Mali