Muda Haumsubiri Mvivu

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Katika maisha yetu binadamu, jambo la msingi na la kuzingatia ni muda. Lakini ukweli ni kwamba watu wengi huwa hatuoanisha muda na maisha yetu ya kila siku. Kama tunataka mafanikio, yatupasa tuujali muda.
Kumbuka, unapopanga mikakati yako katika kila jambo, usipozingatia muda uliojipangia kutekeleza hilo jambo, ushindi wake huwa ni mgumu sana. Ni vema jambo likipangwa lifanywe kwa wakati uliokusudiwa. Ukiamua kulisogeza mbele jambo ulilokuwa umelipangia muda fulani, mipango yako inaweza kuharibika. Kumbuka, mipango yako ni kama agano ulilokuwa umeliweka lifanyike kwa muda maalumu.
Mara nyingi, ukitafakari na kuchunguza sababu zilizofanya jambo lisitendeke, unaweza ukakuta kuwa sababu kubwa ni uvivu tu. Watu wengi wana na tatizo kubwa la uvivu. . Yakupasa ujue kuwa kuwa unapobadilisha ratiba unakuwa umekinzana na muda na mwisho unajikuta hata kile ulichotaka kukifanya kinashindikana. Inapotokea hivi, mara nyingi huwa tunajipa moyo na kujiliwaza kwa kujiambia kuwa nitafanya siku nyingine au wakati mwingine. Pamoja na kujiliwaza kote, tayari muda unakuwa umekwisha kutupa mkono. Matokeo yake, unabakia kushangaa maendeleo na mafanikio ya wenzio ambao waliutumia muda wao vizuri. Muda ulioupoteza, katu hauji kurudi tena.
Hebu sote tuchukue muda kidogo wa kutafakari. Tujiulize maswali yafuatayo kwani mwaka ndio unakatika:
- Je umefanikiwa kukipata kile ulichokuwa umekipanga kifanyike mwaka huu? Endapo jibu lako ni “siyo”,
- Je unafikiri ni kwa sababu gani?
- Je utarudia tena mipango ileile ama utaiboresha kulingana na mazingira yako ya sasa?
- Je unafikiri utahitaji msaada wa wataalamu kukuwezesha kutimiza yale uliyokuwa umepanga?
- Je una mkakati ganii kwa mwaka mpya unaokuja?
Majibu yoyote yawayo yatukumhushe kuwa muda na wakati kamwe havimsubiri mvivu. Tuwe makini namna ya kuutumia muda wetu kwa maendeleo yetu. Tukumbuke kuwa muda ni mali, tukiutumia vizuri unaweza kututajirisha.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania