Jungu Kuu Halikosi Ukoko

Simulizi
by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).
Jungu kuu ni kile chungu kikubwa sana ambacho hutumiwa kupikia chakula cha karamu ya watu wengi sana. Yaani hata watu wawe wengi kupindukia, jungu hilo likipakuliwa lazima litabaki na ukoko. Ukoko ni kile chakula kilichoganda kwenye hilo jungu, na watu wengine huwa wanapenda sana ukoko kwani huuona kuwa ni mtamu, wakati mwingine, kuliko hata chakula chenyewe kilichogandisha ukoko huo.
Usemi huu hutumiliwa sana kwa watu ambao ni wazee. Inaaminika kuwa wazee hawakosi akili ama busara za kufanyia jambo ama busara za kuweka akiba. Kwa maana hiyo, watu, hususani vijana, wanaaswa kutowadharau wazee bali wawe tayari kwenda kwao kwa kupata ushauri na hata kupata msaada. Yatupasa kuwaona wazee kama hazina ya busara na ushauri ambao wanaweza kuutoa wakati wowote endapo watafuatwa na kuombwa wafanye hivyo. Wazee wana kisima cha ushauri na busara kisichokauka. Endapo watakuwa wamepungukiwa ama kukosa kabisa kile wanachoombwa kwa wakati ule, wataweza kuonyesha njia ya kupita ili kuupata ushauri ama msaada unaoombwa. Cha msingi ni kuwa hutakosa kabisa kupata utakacho ama kupewa njia mbadala ya kuweza kupata kile unachohitaji.
Ndio maana watu husema, uzee ni dawa. Tuitumie dawa hiyo pale tunapohitaji, ni muhimu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.
#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Arts #Culture #Tanzania