Usifungue Mlango Wa Moyo Wako Kwa Kila Mtu

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Hapa duniani kila mtu ana ndugu, rafiki, na watu wengi wanaomzunguka. Makundi haya yote yana umuhimu kwa nafasi na wakati tofauti. Pamoja na umuhimu wa hayo makundi, yatupasa tuwe makini katika kuishi nayo. Kuna wakati makundi haya yana umuhimu na yanaweza kuwa ya msaada kwako. Lakini kuna wakati yanaweza kuwa ni mwiba mkali na hivyo kukuharibia maisha yako. 

Marafiki wengi sio wazuri. Tumeshuhudia matukio mengi ya vijana wetu kunyang'anyana wapenzi. Mara nyingi imetokea kuwa yule yule uliyemuamini na kumueleza habari/siri zako ndiye anayeweza kukufanyia ubaya. Kutokana na kufanyiana ubaya, wengi wameishia kupata matatizo ya kiafya, ikiwa ni pamoja na afya ya akili. 

Ukifuatilia kwa makini na kujiuliza kwa nini mambo yako yanakwendea mrama/kombo, unakuta kuwa tatizo ni wewe mwenyewe. Ukijiuliza, ki vipi? Jibu unalipata kuwa uliyaweka bayana mambo yako, ukifikiria kuwa huyo unayemwambia ni rafiki yako. Ulimuamini sana na ukamfungulia mlango na kumweleza yako ya moyoni ambayo sasa yamekuwa shubiri kwako. 

Kuwa makini, angalia na utafakari kwanza kabla hujaamua kutoa habari zako kwa mtu yeyote. Kumbuka, hakuna siri ya watu wawili. Si vema kuanika mambo yako kwa kila mtu. Yakupasa uchukue tahadhari.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Furaha Yako, Machozi Yao

Next
Next

Ukishindwa Hili Leo, Kesho Utashinda Lile