Hata Uwe Mwema Kiasi Gani, Wengine Watakuchukia Tu

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana. Wengine hata hudiriki kusema “Binadamu ni kiumbe mzito.” Hata mtu angekuwa ni mwema kiasi gani hawezi kukosa maadui ama watu wa kumsema vibaya. Hii ni kwa sababu kila mmoja huwa na tafsiri yake kuhusu wema wa mtu, pamoja na wema wako.

Unaweza kumfanyia mtu wema, ukamnunulia nguo nzuri, kama kitenge cha wax, na ukachukua jukumu la kumpelekea kule kijijini kwake aliko. Badala ya kuona na kukushukuru kwa wema wako, huyo jamaa uliyemzawadia, anaweza akakichukua kitenge hicho na kwenda nacho kwa mganga ili akufanyie madawa mabaya, madawa ya kukudhuru. Mtu wa namna hii, moyoni mwake anautafsiri wema wako kama mtu unayejifanya kuwa una hela sana na hivyo yeye anaona kuwa ni bora akukomeshe, akuumize na hata ikiwezekana, akupoteze kabisa. Na hiyo ndiyo itakuwa furaha yake.

Hali kadhalika, unaweza kuwa na mazoea ya kumsaidia mtu, lakini siku ukikwama ukashindwa kumsaidia, usishangae kumsikia akianza kukutangaza kwa watu kuwa wewe ni mchoyo, hujali na pia unaringa sana. Hakuna jema kwa mwanadamu. Kila wakati, binadamu ni mtafuta sababu tu.

Hawa ndio binadamu tunaoishi nao, tunahitaji kuwa na moyo wa chuma ili tusiumie. Tunapaswa kuwa na ngozi nzito na nene kama ya mamba ili tusiumie kiurahisi.

Wakati mwingine yatupasa kufumba macho na kuziba masikio ili kukwepa bugudha kutoka kwa binadamu wenzetu. Hii ni kwa sababu, ukiwaendekeza na kuhangaika nao ili uweze kuwaridhisha hutakaa uendelee ng’oo🤷🏽‍♂️ Utabaki na roho hiyo hiyo ya kutaka kuwafurahisha watu ili wakuone kuwa wewe ni mwema.

Wapende binadamu lakini watakapokuudhi usishtuke na wala usishangae sana. Cha msingi, usikate tamaa, wewe songa mbele tu. Hatima yako na mwisho wako anaujua yule aliyekuumba.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Ujana Ni Kama Maji Ya Moto Kwenye Chupa Ya Chai

Next
Next

Habari Zako Njema Zaweza Kuwa Mbaya Kwa Wakuchukiao