Mwenda Pole Hajikwai

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika maisha, tunatakiwa tujiwekee mipango mikakati ili kujitimizia malengo yetu. Mipango hiyo inaweza ikafanikiwa kwa wakati lakini hiyo haitokei mara zote. Mara nyingi mambo huwa yanachelewa kutendeka kufuatana na mazingira tuliyomo. Kuchelewa kufanyika huwa ni kikwazo kwa wengi. Kuna wale ambao hufikia hatua ya kukata tamaa kabisa. 

Yatupasa tukumbuke kuwa mambo mazuri hayataki haraka. Inatakiwa kuwa na subira katika jambo lolote. Mfano, TEWWY tulianzia mbali, tulikuwa tunaona jinsi tulivyokuwa tunafanya, na mambo yalikuwa yanatuendea vizuri. 

Hapo kati, na hadi sasa, tunaweza kusema, tunapitia kipindi cha mpito. Tunatakiwa tusikate tamaa na kuona kuwa ndio tunafutika kwenye orodha ya Wanaharakati wa Afya ya Akili nchini. La hasha, TEWWY bado ipo na itaendelea kuwepo na kwamba, tunakoelekea ni kuzuri, na pia tutambue kwamba Aliye Juu ameona uvumilivu wetu kutokana na kazi tunayoifanya ambayo inamlenga mhitaji. 

Ni sawa kabisa tukirejea kwenye ule usemi wa mwenda pole hajikwai bali anachelewa tu kufika aendako. Tunamuomba Mungu atusaidie, Mungu isaidie TEWWY ili tuweze kutimiza malengo yetu. Tuko pole pole, tutafika, na hata tukijikwaa, tutasimama kama vile ambavyo tumekuwa tukifanya. Tumedhamiria kuisaidia jamii kwenye masuala ya afya ya akili kwani “Hakuna Afya, Bila Afya ya Akili”.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mla Mla Leo, Sio Mla Nawe

Next
Next

Kulia Ni Tiba