Mteja Ni Mfalme

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Wateja ni msingi na ni sababu ya mafanikio katika biashara yoyote ile. Usemi wa ‘Mteja ni Mfalme’, unaeleza yote. Inaweza kukuchukua miezi mingi kumpata mteja kwenye biashara yako. Hali kadhalika, inaweza ikakuchukua sekunde moja tu, kumpoteza mteja. Haya yamewakuta wengi tu.

Usipowajali wateja wako, mtu mwingine atawajali zaidi. Mteja wako katika biashara zako ndiye lengo lako, hivyo huna budi kumjali. Inatulazimu kuwapatia wateja wetu huduma bora na si bora huduma.

Yatupasa tufahamu kwamba tukiwapa huduma bora wateja wetu, siyo rahisi kutusahau, ama kutukimbia. Badala yake, watatutangaza kwa wengine pia na hivyo kupanua wigo wetu wa wateja. Tujitahidi sana na ni jambo muhimu kuwa na mahusiano mazuri na wateja wetu.

Tumtendee vema kila mteja kana kwamba ni mteja peke yake duniani hapa ili aweze kuitangaza biashara yako kwa watu wengine. Ni jambo la busara sana kuongeza wateja wapya lakini pia hakikisha huwapotezi wateja wako wa zamani. Kumbuka, biashara ni wateja.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Uliza, Usitete

Next
Next

Kidole Kimoja Hakivunji Chawa