Mipango Ni Dira Ya Mafanikio

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Katika maisha, unahitaji kuwa na mpango au picha ya unakotoka na unakotaka kwenda. Ukishindwa kupanga ina maana umeamua kushindwa kwa sababu utakuwa huna taratibu zozote za kukuongoza njia ya kupita katika safari yako. Kuna msemo usemao, "kama huna dira ni kama meli iliyoko baharini bila kujua inaelekea bandari gani". Itakuwa ni vigumu kwa meli hiyo kufika sehemu tarajiwa.
Maisha ni mapambano yanayohitaji maandalizi. Tunachotakiwa kufanya ni kubuni mpango wa maisha yako na sio kuishi kwa kutegemea mipango ya watu wengine. Ukiwa na mpango, utakusaidia kujua unakokwenda, na utaweza kupima maendeleo uliyofikia. Binadamu yeyote anapaswa kuwa na ndoto ya anachotaka kupata katika maisha yake hapa duniani. Mipango unayoiweka, inatakiwa iendane na ndoto yako ambayo unaamini kuwa itakuletea matokeo ya aina fulani.
Wataalamu husema, “Kupanga, ni Kuchagua”. Lakini, pamoja na uhalisia wa usemi huo, ili kuwe na maana, ni muhimu sana kuhakikisha kuwa unatekeleza yale ama kile ulichopanga. Kumbuka, kuishi bila mipango kunaonyesha kuwa wewe hapa duniani upo upo tu, na kwamba uko tayari ama unapanga kushindwa. Kama unapanga kushindwa, ina maana basi kuwa umekata tamaa.
Binadamu hatutakiwi kuwa hivyo, hatutakiwi kukata tamaa. Safari yetu ni fupi sana hapa duniani na hivyo yatupasa tuwe na mipango ili tuwe na sababu ya kuishi kwenye safari hii fupi yenye changamoto nyingi za maisha.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection