Kwa Mpumbavu, Neno Msamaha Halina Maana

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Upumbavu ni sifa. Sifa hii hupewa mtu ambaye huwa hayuko tayari kukubali ama kuelewa kile anachoambiwa ama kushauriwa na wenzie. Hivyo, mtu mwenye sifa hii ya upumbavu huitwa mpumbavu.
Utamtambuaje kuwa mtu huyu ni mpumbavu? Ni rahisi sana kumtambua mtu aliye mpumbavu. Pale utakapokuwa umemkosea makucha yake ya upumbavu yatajitokeza. Kwa vile utakuwa umemkosea, kama ilivyo kawaida, utajitahidi kumuomba msamaha ili yaishe. Lakini yeye hataelewa wala hatakusikia na kuutilia maanani msamaha unaouomba. Badala yake ataendelea kulalama na kuona kuwa ameonewa. Kwa upumbavu wake, ataendelea kusambaza kwa watu yale anayoyaona yeye kuwa amekosewa. Uwezo wake lakini ni ule wa kuwasambazia watu wa aina yake, yaani wapumbavu wenzie ambao hawana uwezo wa kupambanua mambo. Hivyo basi, hao nao wataendelea kumchochea zaidi na hivyo kumfanya hasira zake zipande zaidi.
Kutokana na kuchochewa huko, itakuwa kila unapokutana naye, atakuwa anakumbuka kile ulichomfanyia kwani anakuwa bado hajasahau na zaidi ya yote anakuwa bado hajasamehe, pamoja na kuombwa kote alikoombwa kuwa asamehe.
Kwake yeye, jambo hilo linakuwa bado halijaisha. Hata ukijaribu kurudia tena kumsihi na kumwomba kuwa yaishe, eti bado utakuwa unampandisha hasira. Mwisho wa siku utapata jibu kuwa mpumbavu hajui kusamehe, na kwamba huwa hasahau kamwe.
Wako watu wengi wa aina hii ambao wanashauriwa kubadilika. Kukoseana ni jambo la kawaida. Asiye kosea ni Mungu peke yake.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection