Akumulikaye Mchana Usiku Hukuchoma

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maadam tunaishi hapa duniani, tunakutana na marafiki wazuri, wabaya, wanafki, wambea na wengine wengi tu. Kwa mfano, rafiki yako unayemwamini sana anaweza kukutania, kukutishia au kukusema vibaya hadharani, yaani waziwazi, lakini kwa kuwa ni rafiki yako mmeshibana, unaona ni utani au kawaida tu, na unaweza ukamchukulia poa.

Kumbe katika yote hayo rafiki yako alikuwa hakutanii, alikuwa anamaanisha kweli kweli. Siku ya siku yale yote aliyokuwa anatania yanatokea kiukweli, wewe unabaki unajiuliza 'hivi huyu rafiki yangu anaweza kunifanyia jambo zito kama hili kweli au naota?'

Kumbe alishakuonyesha ishara mapema ila hukumwelewa bali uliona ni utani au kawaida tu. Laiti ungalitafakari vizuri kabla, hayo yote yasingelitokea kwani kinga ni bora kuliko tiba. Lakini pia jiulize kama rafiki yako anakusema waziwazi ukiwepo, je kama haupo si ndiyo atasema mazito na mabaya zaidi? 

Hii inatufundisha kuwa makini na marafiki zetu, tusiwaamini mia kwa mia pia tusidharau, wala kupuuza maongezi yao hata kama ni utani. Yatupasa tuyatafakari kwa kina ili baadaye yasije geuka na kutuumiza.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Kushindwa Ni Sehemu Ya Maisha

Next
Next

La Kuvunda Halina Ubani