Usiingilie Mazungumzo Ya Watu

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kuna watu katika maisha yao huwa wanapenda sana kuonekana wanaelewa sana habari nyingi za watu. Watu hao mara zote huwa wakiwakuta watu wako kwenye maongezi yao, lazima watajitahidi kuonyesha kuwa wanakijua hicho wanachoongea. Hapo hapo, huanza kuchangia bila hata ya kujua mazungumzo hayo yalianzia wapi. Tabia hii huwa siyo nzuri hata kidogo, inaweza kukuponza.

Alikuwepo kijana mmoja ambaye alikuwa fundi sana wa tabia hiyo ya kujichomeka kwenye mambo ama mazungumzo yasiyomuhusu. Ikawa siku moja katika pita pita zake akawakuta vijana wenzake wapo mahali, wanaongea kuhusu habari zao. Bila kuchelewa, naye akajiunga nao. 

Kumbe maskini, wale vijana walikuwa wanatafutwa na polisi kwa kesi ya uhalifu. Punde kidogo, wote wakakamatwa na kuwekwa rumande. Kesi ilipelekwa mahakamani. Maamuzi ya kesi, ilikuwa hao vijana wafungwe miaka mitano mitano. Huyu kijana naye alikuwa mmoja wao kwani pamoja na kwamba hakuhusika, alikutwa kwenye kundi hilo. Kijana alilia kwa uchungu lakini machozi yake hayakusaidia kitu, yalikuwa ni bure. Adhabu ya kwenda jela ilimhusu pia. Kisa kikiwa kupenda kuingilia mambo yasiyomhusu. 

Usemi huu unatufundisha tusiingilie mambo tusiyoyajua na yasiyotuhusu. Tukikuta watu wanaongea habari zao, hatuna sababu ya kuwaimgilia. Kama watakualika ili ujumuike nao, waweza fanya hivyo, la sivyo iwe ni mwiko kabisa. 

Yatupasa tuheshimu watu na mazungumzo yao. Tukifuata ushauri huu tutajiepusha matatizo mengi yanayoweza kutokea kutokana na tabia hii mbaya. Yaliyomkuta kijana kwenye simulizi hii ni fundisho tosha kwetu sote.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Sio Sahihi Kila Mtu Kujua Changamoto Zako

Next
Next

Hakuna Tajiri Anayemjali Maskini, Na Hakuna Maskini Anayemhurumia Tajiri