Wizi Wamsababishia Upofu

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Upofu ni hali ya kupoteza uono. Vipo vyanzo mbali mbali vinavyosababisha upofu. Baadhi ya vyanzo hivyo ni pamoja na ajali, magonjwa ya kurithi na ya kuambukiza. Kuna wakati mwingine, chanzo kinaweza kutokana na tabia mbaya ya mtu, mathalani, wizi.

Hapa nitasimulia tabia mbaya ya wizi. Kulikuwepo na kijana mmoja ambaye alikuwa na tabia ya wizi. Alikuwa akiwaibia watu wakiwa kwenye vituo vya mabasi na sehemu nyingine zenye mikusanyiko ya watu. Alikuwa na ujasiri wa kukwapua vitu kutoka hata kwa watu wakiwa wanatembea barabarani. Kwa hakika alikuwa ni mzoefu wa hali ya juu sana. Watu waliibiwa na kijana huyu hata wakiwa ndani ya basi. Kwa kweli, alikuwa ni wa hatari sana. Wazazi walimkanya sana aache tabia hiyo, lakini maneno yao yaligonga mwamba. Hali kadhalika, jamii inayomzunguka, ndugu, jamaa na wote waliokuwa na mapenzi mema walijitoa na kuwa sehemu ya kumkanya kijana huyo, lakini kijana hakusikia la mtu.

Siku moja alikwapua simu ya mtu. Kama watu wasemavyo, “Siku za Mwizi ni Arobaini”, kwa kijana huyu zilikuwa zimetimia. Watu waliposikia tu kelele za mwiziiii, mwiziii walimkimbiza hadi wakamkamata. Hasira zote zilimiminwa juu yake. Mwenye nawe haya, mwenye nondo, haya. Hatimaye waliamua kumtoboa macho yote. Ilikuwa hatari. Pamoja na kwamba alitibiwa, alipona vidonda lakini alipata ulemavu wa kudumu wa kutokuona tena. 

Watu husema ukizoea tabia fulani kwa muda mrefu, siyo rahisi kuiacha. Kwa kijana huyu ilikuwa kweli kabisa. Tabia yake ya wizi ilikuwa kama kilema sasa. Pamoja na kwamba kwa sasa aligeuka kuwa omba omba, kwenye mchakato huo huo wa kuomba omba, tabia hiyo mbaya ya kuiba hakuiacha. Watu wakiwa kwenye foleni au mkusanyiko bado aliendelea kuwachomolea pochi zao au chochote alichoweza kuweka mkono wake. Watu wanajiuliza, bila macho ya kuona, aliwezaje kujua wapi atie mkono wake ili aweze kutoka na chchote!! Ni ajabu na kweli.

Simulizi hii inatoa fundisho kwa vijana kuwa maisha hayana njia ya mkato, ni lazima kufanya kazi ili mkono uende kinywani. Pia vijana wanaaswa kuacha uvivu. Yawapasa wafaye kazi ili waweze kujikwamua kimaisha. Hata vitabu vitakatifu vimeandikwa, asiyefanya kazi na asile. Madhara ya kuwa mwizi ni makubwa sana na wengi wamefikia pabaya kwa kuwa na tabia hizo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Nimekupaka Wanja Wewe Umenipaka Pilipili

Next
Next

Machozi Ni Kiwakilishi Cha Hali Ya Uchungu Ama Furaha