Ahadi Ni Deni

Avelina Hokororo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Avelina Hokororo (Wisdom&Wellness Counselor – TEWWY).

Deni ni kitu chochote ambacho umechukua kutoka kwa watu na unakuwa bado hujalipa. Deni linaweza kuwa ni pesa au kitu chochote ulichoazima kutoka kwa mtu huku ukiahidi kuwa utalipa ama kurudisha kwa wakati mliokubaliana. 

Ahadi inatokana na kuahidi kutoa kitu na kisha kulipa baadaye. Nataka kusema kuwa katika maisha, ukiahidi na usipotekeleza, unakuwa umejitoa kwenye utu wako. Pia unakosa amani maana linakuwa deni ambalo linaweza kukufikisha mahakamani. Uzuri moja wa deni lakini ni kwamba, likifika mahakamani halikufungi. Mahakama itaamua kuwa itakupasa ulipe hilo deni lote hadi liishe. 

Hali hii inaweza kuwa ya fedheha kwako na watu wanaweza kukuita majina mengi. Mathalani, unaweza kuitwa tapeli, mwizi, laghai n.k. Imani ya watu kwako itatoweka kabisa na hautaamimika tena. 

Kutokana na andiko hili, tunajifunza kuwa yatupasa tuepuke kuahidi mambo ambayo hatuwezi kuyatekeleza. Mara nyingi ahadi huwa zinatolewa kwenye mihadhara kama vile ya sherehe. Pengine wakati unapotoa ahadi unakuwa katika hali ambayo inakufanya uahidi chochote kile, bila kufikiri. 

Tunashauriwa kuwa waangalifu sana tunapotoa ahadi. Tusiahidi kama tuna furaha sana ama kama tumelewa. Hali kadhalika, tunatakiwa tusiahidi tukiwa tumekasirika au tukiwa katika hali ya kutojitambua. Ni vema kuchukua tahadhari kwani, utakaporudia hali yako ya kawaida unaweza ukaja shindwa kutekeleza ahadi hizo na watu, hawatakuelewa. Badala yake utajisababishia sonona, kwani utakuwa unabadilisha njia au kujificha mara kwa mara kwa kuogopa kudaiwa. Na wengine hufikia hata hatua ya kujitoa uhai kwa sababu ya madeni. Adha ya madeni ni mbaya sana. Kwa kadri ya uwezo wetu, tujaribu sana kuyakwepa madeni. Pale tutakapo kopa, basi shime tukumbuke kulipa kama tulivyoahidi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Upendo Unaweza Kuwa Wa Kinafiki, Chuki Huwa Ni Halisi

Next
Next

Nimekupaka Wanja Wewe Umenipaka Pilipili