Usitunze Huzuni Moyoni

Masimulizi
by Suzanne Njana (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Huzuni ni hali ya masikitiko yenye masononeko inayomfanya mtu akose furaha, amani na matumaini kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu. Hali hiyo humfanya mtu atawaliwe na mawazo mengi sana, ikiwa pamoja na msongo wa mawazo na sonona. Inapokithiri bila kupata huduma sahihi huweza kusababishahta kifo.
Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha mtu kuwa na huzuni. Baadhi ni kufiwa, kuachwa na mpenzi, mume ama mke, kutengana kwa wana ndoa, kudhulumiana, migongano na migogoro katika familia, hali ya kukosa kipato cha kujikimu kimaisha, kukosa kazi, ajali, kutojituma kufanya kazi (kuchagua kazi) au changamoto mbalimbali katika maisha.
Simulizi hii inatukumbusha kuwa, tunaweza kuepuka hiyo hali ya msongo wa mawazo na sonona kwa kuzingatia baadhi ya mambo yafuatayo:
- Kumshirikisha mtu wako wa karibu changamoto unazopitia, kamwe usikae nazo moyoni, zitakuumiza.
- Kumshirikisha Mnasihi aliye karibu nawe ili akupatie huduma ya unasihi.
- Kujituma kufanya kazi unayoweza, usichague kazi.
- Kutokata tamaa katika maisha, kuvumilia hadi kufanikiwa.
- Kijitahidi kuwa na mtizamo chanya kwako mwenyewe na hata kwa shughuli zako.
- Kuchangamana na wenzako kwa kushirikiana nao katika nyanja mbalimbali.
- Endapo hali itakuwa mbaya sana Mnasihi atakupa rufaa ya kumwona Daktari hospitalini.
Hivyo usikubali kutunza huzuni (changamoto) moyoni mwako kwani zinaweza kukusababishia athari nyingi katika maisha. Ukizingatia hayo naamini huzuni haitakuwa fungu lako.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection