Usitoe Maamuzi Wakati Una Furaha Sana

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tuko katika ulimwengu wenye vurugu na fujo zisizohesabika. Kila mtu anacho akijuacho ambacho anaona mwingine hakijui na wala hakiwezi. Ni fikira ambazo wanadamu tunatembea nazo. Furaha na huzuni ni sehemu ya maisha yetu.
Unapokutana na jambo la kuhuzunisha unatamani dunia isingekuwepo na zaidi unaona kwa nini yakupate wewe. Lakini mtu huyo akiwa katika furaha hata lugha yake inabadilika. Atatamani kila mtu ajue kuwa yeye ni nani hasa kama pana mabadiliko ya uchumi. Popote atakapokuwa atataka yeye awe msemaji mkuu na mwenye kutoa maamuzi. Anaweza hata akaahidi jambo ambalo hataweza kutekeleza kutoka na na uwezo wake. Majigambo mengi baadaye huleta huzuni pamoja na aibu. Furaha yake ni kujijengea jina na kujitangaza, na si vinginevyo.
Watu wa aina hii huwa mwisho wake ni mbaya, hasa pale anapokuwa ameshindwa kutekeleza kile alichoahidi. Mchezo wa majigambo upo sana kwenye mikusanyiko ya maandalizi ya sherehe mbalimbali. Mara nyingi utakuta mtu anaahidi, siyo kwa uwezo, bali kwa kuwaiga wengine na kwa zile furaha alizokuwa nazo mahali hapo.
Mwisho wa siku anaingia mitini kwani anauona mzigo aliojibebesha kwake ni mzigo mzito. Alijibebesha mzigo huo kwa kutaka sifa, kumbe hana ubavu huo.
Sambamba na usemi huu, tunatakiwa tusiige ya fulani tusije tukaangamia. Maamuzi yetu tusiyatoe tukiwa tumefurahi, kwani tunaweza tukajikuta tunayafanya bila ya kuwa makini. Tufanye maamuzi ya busara.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection