Mtu Hufurahia Shida Zako, Sio Furaha Yako

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Matatizo yameumbwa na kila mtu huyapata. Hakuna mtu ambaye hajawahi kupitia matatizo, na hayuko ambaye hatayapitia. Inategemea ni tatizo gani na wakati gani linakutokea.
Katika kipindi hiki cha matatizo ndipo utakapomfahamu mtu ambaye yuko na wewe, mwenye dhamira nzuri nawe. Uhalisia wa watu hujulikana pale utakapokuwa na matatizo. Walio wengi, hata kama ni marafiki zako wataanza kukukwepa na kukusema vibaya. Watu husema, ogopa sana ngulu mbili/wanadamu kwani hawaaminiki kabisa, huweza kugeuka wakati wowote.
Kuna mfano halisi ambao napenda kuwashirikisha wasomaji. Kuna ndugu yangu moja ambaye alikuwa na roho nzuri sana na alipenda kusaidia watu. Alikuwa mkaribishaji mzuri sana wa watu nyumbani kwake. Pia aliishi kwa kuwasaidia watu wengi waliohitaji msaada wake, pamoja na kuwatafutia kazi.
Bahati mbaya alipata matatizo kazini, akafukuzwa kazi. Wakati akiwa kazini, alikuwa ni mtu wa msaada kwa kila mtu. Wengi walipata kazi kupitia wema wake. Hao aliowasaidia kupata kazi walikuwa wana bahati sana kwani kazi zao zilikuwa ni nzuri. Wakati akiwa na kazi, watu wengi walikuwa na mazoea ya kwenda nyumbani kwake.
Amini usiamini, baada ya kugundua kuwa hana kazi walikata mguu, wakawa hawapiti kabisa nyumbani kwake. Kwa kuwa aliachishwa kazi kutokana na makosa aliyoyafanya, hakuweza kulipwa chochote. Maisha yake yalibadilika sana, akawa na maisha magumu isivyoelezeka. Kwa hakika hali ilibadilika sana. Watoto wakawa hawaendi shule tena kwa kuwa walikuwa wakisoma kwenye mchepuo wa kiingereza.
Alianza kuwatafutia watoto wake shule hizi za kawaida, wengine huziita shule za Kayumba, nazo pia akawa hapati. Cha ajabu, wale aliokuwa akiwasaidia enzi zile alipokuwa na nafasi nzuri, sasa walikuwa wanamdhihaki na kufurahia hiyo hali yake aliyokuwa nayo sasa. Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana. Ukifurahia matatizo ya mwenzio, kwani wewe unapata nini? Ni roho ambazo zimesheheni ubaya mtupu.
Simulizi hii inatufundisha kuwa tuwe na kiasi katika kusaidia watu kwa sababu, katika kumi uliowasaidia, huenda ni mmoja tu ataweza kurudi kukushukuru kwa kile ulichomfanyia. Hakuna mtu anayefurahia kupata kwako ila pale tu anapokuwa anahitaji msaada kutoka kwako. Binadamu wengi huogopa kuambiwa wana roho mbaya pale wanapowakatalia kuwapa watu misaada. Tusiogope kuambiwa kuwa tuna roho mbaya kwani shukrani za punda huwa ni mateke.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection