Ishi Kadri Unavyojaliwa, Na Sio Kama Mwingine Anavyoishi

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Watu wengi wana kawaida ya kupenda kujilinganisha na watu wengine. Watu kama hao hupenda kujiuliza,  “kama yule yuko hivi, kwa nini na mimi nisiwe vile?”

Wanadamu tunatakiwa kuishi kufuatana na mipango ambayo tunakuwa tumejipangia. Kwa maana hii, mpango wa yule hauwezi kuwa sawa na mpango wa kwako. Endapo utakuwa na tabia ya kuiga na kuangalia ya wengine, maisha hutayaweza na hivyo lazima utafika mahali pa kushindwa. 

Acha kushindana na watu. Angalia ya kwako, yale yanayokuhusu wewe. Usipende kuangalia ya wenzio. Kila mtu Mungu amemjalia kilicho chake kwa kadri ya uwezo wake. Mzigo wa mwenzio huwezi kuubeba na utakapolazimisha kuubeba, unaweza ukashindwa kuushusha. Kumbuka hata vidole vina ukubwa tofauti lakini vinashirikiana katika utendaji wa kazi.

Ishi kwa kile Mungu alichokuwezesha na kukujalia. Kamwe usiangalie jinsi fulani anavyoishi, haitakusaidia zaidi ya kukupa ugonjwa wa moyo. Pambana na hali yako, ili ufikie hatma yako. Usipende kufanya kwa sifa, ili watu wakuone. Fanya kwa ajili yako na wale wanaokutegemea. Huo ndio utaratibu mzuri wa maisha.

Usemi huu unatufundisha tabia ya kupenda kutegemea akili zetu na ufahamu wetu zaidi kuliko kuiga iga wengine na kutaka tufanane ama tuwe kama yule, hiyo haitawezekana kamwe. Wewe ni wewe, na yule ni yule. Hata ufanyeje, huwezi ukawa kama yule. Ridhika na hali yako.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mtu Hufurahia Shida Zako, Sio Furaha Yako

Next
Next

Tujifunze Kusamehe