Tujifunze Kusamehe

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Alikuwepo mama mmoja ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Mama huyu alibahatika kupata mtoto wa Kike ambaye aliweza kumsomesha hadi Chuo Kikuu. Baada ya kuhitimu shahada yake, alimtafutia kazi nzuri.

Siku moja mama alimtuma bintiye kwenda sokoni kununua mahitaji ya nyumbani. Binti alitekeleza kama alivyoagizwa na akaongezea pesa yake kwa ajili ya kununua baadhi ya mahitaji ya ziada ambayo aliyaona kuwa ni ya muhimu.  

Aliporudi nyumbani aliorodhesha vitu vyote alivyonunua na bei zake. Halafu bila aibu alimwambia mamake, "Mama ninakudai kiasi fulani cha pesa ambazo zilipelea ikabidi niongezee”. Binti akaweka ile karatasi mezani sebuleni ili mama akirudi aisome. 

Mama aliporudi hakuisoma, aliingia chumbani moja kwa moja na kwenda bafuni. Binti alipoona mama hajaisoma akaiingiza chumbani fasta akaiweka kitandani.

Mama alipotoka bafuni akaiona ile karatasi, akaisoma kisha akaigeuza upande wa nyuma na kumjibu binti kama ifuatavyo:

“Mwanangu ahsante kwa ujumbe. Ila ningependa nami nikueleze machache”:

1. Nilipopata ujauzito wako, ilinigharimu hela nyingi kuilea mimba hadi kuzaliwa kwako. Kutokana na matatizo niliyokuwa nayo, ilibidi nipumzishwe hospitalini kwa miezi kadhaa. Lakini sikudai chochote, kwani nimekusamehe.

2. Nilipokuzaa nilipata matatizo makubwa sana, isitoshe wewe pia uliugua kwa muda mrefu. Ilinilazimu kutumia gharama kubwa sana kukutibia. Lakini, pia sikudai, nimekusamehe.

3. Nilikununulia nguo nzuri za gharama kubwa na kukulisha vizuri hadi ulipoweza kujihudumia mwenyewe, bado sikudai chochote mwanangu, ila nimekusamehe.

4. Nilikusomesha kwa gharama kubwa tangu chekechea hadi Chuo Kikuu na bado sikudai, nimekusamehe.

5. Nimekutafutia kazi nzuri lakini sikudai mwanangu, nimekusamehe.

Mama akaweka karatasi juu ya meza sebuleni. Binti akasoma ile karatasi akamwambia mama yake, "Mama nisamehe, kwani gharama unazonidai ni pesa nyingi sana kuliko ninazokudai”. Nimejifunza mengi kutoka kwako mama, nakushukru. Nami kuanzia leo sikudai hata senti moja, hivyo mama yangu nami nimekusamehe kama ulivyonisamehe.

Hapa tunajifunza kuwa, kusameheana ni jambo jema na la msingi katika maisha kwani linarejesha upya amani, upendo na furaha kati ya familia, ndugu, marafiki na hata jamii. Sote yatupasa tujifunze kusamehe kwani hakuna mwanadamu aliyekamilika.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ishi Kadri Unavyojaliwa, Na Sio Kama Mwingine Anavyoishi

Next
Next

Njia Ya Mkato Tamu, Lakini Ina Madhara