Ukubwa Ni Jaa

Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY)

Simulizi

by Tap Elderly Women's Wisdom for Youth (TEWWY).

Jaa ni jalala, mahali ambapo watu hutupa taka taka zao. Kwa hiyo mtu mkubwa ni kama jaa, kila mwenye takataka zake, (matusi, lawama, n.k) humtupia yeye.

Usemi huu hutumiwa kuwakumbusha watu wenye vyeo na madaraka, mathalani, viongozi. Wanashauriwa kuwa wasikasirike wanaposhambuliwa na wanapolaumiwa na watu kutokana na sababu mbali mbali. Hii ni kwa sababu, ukubwa si raha, ni sawa sawa na jaa. Kila mwenye taka taka zake huenda kuzitupa hapo. Haijalishi ni taka taka za aina gani, cha msingi kujua ni kuwa ni uchafu unaotupwa kwenye jalala lako kutokana na ukubwa ama cheo ulicho nacho..

Mtu akiwa na cheo cha kuongoza watu, yampasa awe tayari kwa kila jambo, liwe zuri ama baya. Wakati anafurahia raha za ukubwa ni lazima pia awe tayari kubeba mambo yote yanayoweza kutokea. Huo ndio mshahara wa ukubwa, siyo pesa peke yake.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Hakuna Marefu Yasiyokuwa Na Ncha

Next
Next

Adui Hatoki Mbali