Tafuta Raha, Shida Zinakuja Zenyewe

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Neno shida lina maana pana sana. Tunaweza kusema kuwa shida ni tatizo ambalo mtu anakuwa nalo. Mtu anaweza asijue namna ya kujinasua au namna ya kufanya ili aondokane nayo.

Ziko shida za aina nyingi, mathalani, shida ya kufiwa, kuuguliwa ama shida nyingine yoyote ile. Ukweli ni kwamba, shida halitafutwi bali inakuja tu bila ya taarifa ama mapatano. Mara nyingi shida huja wakati huna jinsi ya kutatua. Ndipo unapohitaji kusaidiwa ili utoke katika ile hali. Shida haina hodi kabisa nahivyo haingoji karibu.

Tukija kwenye eneo la raha, hapo lazima uitafute kwa namna yeyote ile. Lakini ieleweke kuwa, raha haiji kwa mtu anayependa kubweteka bweteka tu. Unapotafuta raha, utapambana kwa nguvu zako zote na namna zote ili uweze kufanikiwa. Kwa maana hiyo, bila kupambana, raha utaisikia kwa wenzio. Yakupasa uhangaike hapa na pale ili upate matokeo mazuri, upate kile ukitakacho.

Hii ni kusema kuwa, raha inatafutwa kwa udi na uvumba, lakini shida haitafutwi. Shida inakuja yenyewe bila kuitwa wakati raha inakuja kwa kutafutwa na inakuja kwa wakati na majira yanayoruhusiwa. Ndio maana wahenga walinena kua, 'Mtaka cha Uvunguni Sharti Ainame". Kamwe tusitegemee kuwa raha zitatufuata bila kuhangaika, hii ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii zote.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Akufaaye Kwa Dhiki Ndiye Rafiki

Next
Next

Usiogope Kuchukiwa, Ogopa Kulaumiwa