Heri Lawama Kuliko Fedheha

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Lawama ni hali ya kulalamika kuhusu jambo ama tatizo fulani. Fedheha maana yake ni aibu. Mara nyingi watu hutumia muda wao mwingi kulalamikia ugumu wa maisha. Ukiwachunguza watu hao kwa undani utakuta ni wale ambao ni wavivu, wasiopenda kufanya kazi. Mara nyingi watu hao hushinda vijiweni na kuzungumza mambo ya umbea ambayo hayana tija kwao wala kwa jamii. Kati ya watu hawa huwa na dharau na kebehi, wasiotafuta fursa, wasiopenda kushirikiana na wenzao na wenye mtizamo hasi dhidi ya wenzao na wao wenyewe.
Ukweli ni kwamba, katika maisha yatupasa tuwe na msimamo na tuwe na maamuzi ya kufanya mambo tunayoyaamini, mambo yaliyo sahihi na yenye uhakika. Haitasaidia kuacha kufanya kabisa au kuhofia kuwa wabaya wako watakulaumu.
Kulaumiwa kutakuwepo kila siku, hata ungefanyaje. Kama ukilaumiwa, malalamiko yao hayatakuwa na mashiko kwani jambo lako utakuwa umelifanya na cha msingi, litakuwa linaonekana.
Kwa wale wanaopenda kulalalamika na kusema maisha ni magumu na kulaumu wenzao, tunaweza kusema kuwa hawana busara. Kukaa na kuogopa kufanya shughuli zako kwa sababu zisizoeleweka vizuri, na za kubahatisha, hatma yake ni kupata aibu.
Simulizi hii inatufundisha kuwa yatupasa kutenda jambo unaloliamini na unalolijua. Hutakiwi kuogopa watu wengine watasemaje kuhusu wewe. Watu wana uhuru wa kusema wanachotaka, hiyo isikusumbue.
Hali kadhalika,, tunafundishwa kuacha kulalamika kila wakati. Yatupasa tuache uvivu na umbea. Tujifunze kuwa wabunifu, tufanye kazi kwa bidii, tujitume na tutafute fursa mbalimbali katika maisha yetu. Maisha ni kujituma, maisha ni mapambano. Hakuna fedhea wala lawama katika kupambana na maisha.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection