BAADA YA JUA KUZAMA, WASICHANA HAWARUHUSIWI KUTOKA NYUMBANI KWAO

Grace Mshanga
Wisdom&Wellness Supervisor
Temeke & Ubungo, Dar-es-Salaam
Jua likizama na kiza kikianza kuingia wakati huwezi kumtambua vizuri anayekuja mbele yako, wasichana hawaruhusiwi kutoka nje ya nyumba yao. Hii inawalinda wasichana ili wasitendewe mabaya au kuonewa na wavulana maana wakati huu wavulana huwa matembezini. Pia hii ni njia mojawapo ya kuwafundisha watoto wa kike kuwa na tabia njema.