Usiwaze Yaliyopita Au Ya Zamani, Yatakuchelewesha

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi ...

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Katika maisha yetu tunapitia mazuri na mabaya. Mara nyingi wengi wetu tuna tabia ya kuyakumbuka na kuyatafakari mabaya yaliyopita, lakini hiyo haisaidii lolote zaidi ya kutuongezea machungu na maumivu. Kama wana falsafa wasemavyo, maji yakimwagika hayazoleki, ni kweli kabisa, hata ungekuwa na utaalamu wa namna gani huwezi ukayazoa. Kwa hiyo hatupaswi kuendelea kuruhusu kuwaza makosa tuliyowahi kuyatenda katika maisha yetu ya huko nyuma. Kwa mfano mtu unajikuta unasema laiti ningelijua tangu mwanzo nisingekubali au nisingefanya hayo niliyoyatenda. Maneno yanayoanza na … ningelijua… nisinge... huwa Haya a maana katika maisha ya mwanadamu. Tujifunze kuyafuta na kuyasahau kabisa makosa yetu ya zamani kwa lengo la kuyatazama mema na mazuri yaliyoko mbele yetu. Tuchukue hatua sahihi za kutufikisha pazuri. BUSARA zetu zitusaidie kutumia makosa tuliyowahi kuyafanya kama sehemu ya kujifunza na kutoruhusu makosa mengine tena ili kutengeneza maisha mapya na kuweza kusonga mbele.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Tabia Nzuri Yamnusuru Kifo

Next
Next

Chovya Chovya Humaliza Buyu La Asali