Tabia Nzuri Yamnusuru Kifo

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi ...

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Tabia njema siku zote ni kinga au akiba dhidi ya mambo mabaya yanayoweza kukutokea katika maisha yako baadaye. Katika kuthibitisha hilo, tuone ni jinsi gani msemo huo unavyoweza kuwa na ukweli kama ifuatavyo:

Kulikuwa na baba mmoja ambaye alifanya kazi katika kiwanda cha barafu. Kila siku asubuhi alipokuwa akiingia kazini alikuwa na tabia ya kumsalimu mlinzi wa pale getini. Vivyo hivyo jioni anapotoka alimuaga mlinzi na kuondoka kwenda nyumbani.

Siku moja jioni wafanyakazi wakiwa wanajiandaa kuondoka kurudi makwao, kiwandani kulitokea tatizo ambalo ilibidi yule baba arudi pale kiwandani ili kulishughulikia. Alipomaliza, ghafla umeme ulikatika, milango yote ikajifunga na haikuweza kufunguka. Kwa kuwa kulikuwa hakuna mawasiliano mle ndani, baba huyu alinasa ndani, akashindwa kutoka. Kwa bahati nzuri mfanyakazi huyo alikuwa na tabia nzuri iliyoambatana na mazoea ya kumsalimia mlinzi kila siku asubuhi anapoingia na kumuaga kila siku aondokapo jioni. Kutokana na hali hii, alipokwama ilikuwa rahisi kwa mlinzi kutambua kuwa yule mfanyakazi alikuwa bado hajatoka kwa sababu ilikuwa bado hajamuaga.

Hali hiyo ya kutokumuona yule
baba ilimshitua sana mlinzi. Alianza kuzunguka kiwandani kote kumtafuta na hatimaye alipogundua kuwa umeme ulikuwa umekatika alijua kuwa alikuwa amenasa mle ndani ya kiwanda. Kwa haraka alivunja mlango ili amuokoe yule baba.
Alimpata akiwa bado hai ingawa alikuwa dhaifu sana.

Alimpeleka hospitali ambako alilazwa kwa matibabu. Baada ya siku chache alipona na akarudi nyumbani na hatimaye kurejea kazini akiwa na afya njema.

Kisa hiki kinatufundisha kuwa kila siku katika maisha yetu yatupasa kutenda angalau jambo moja jema, kama kusalimiana na wenzetu kama alivyokuwa akifanya huyu baba. Kwake yeye, utu wake ulikuwa ni akiba ya ukombozi wake wakati alipokuwa amenaswa kwenye kiwanda cha barafu.
Funzo hili linalandana na methali zifuatazo: ‘Wema hauozi, na Akiba haiozi.’

Tujifunze kuwekeza mema kwa faida za baadaye.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Aanguaye Huanguliwa

Next
Next

Usiwaze Yaliyopita Au Ya Zamani, Yatakuchelewesha